Skip to content
Gospo FM Radio 99.1 FM, Ishara ya Upendo

IEBC

26 Novemba 2026

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini IEBC imesema huenda ikashindwa kupeperusha moja kwa moja matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 kutokana na gharama kubwa ya zoezi hilo.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini IEBC imesema huenda ikashindwa kupeperusha moja kwa moja matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 kutokana na gharama kubwa ya zoezi hilo.

Akizungumza jijini Nairobi wakati wa mkutano na wanahabari wanaoripoti masuala ya kisiasa, mwenyekiti wa tume hiyo Erastus Ethekon amesema zoezi hilo linaweza kugharimu mabilioni ya shilingi.

Ethekon amesema tume hiyo italazimika kununua vifaa zaidi ya elfu 50 na pia kutoa mafunzo na kuajiri idadi kama hiyo ya wafanyakazi ili kutekeleza zoezi hilo.

Amesema gharama hizo zinaibua wasiwasi kuhusu uwezo wa tume kutekeleza mpango huo wakati wa uchaguzi mkuu ujao.