Skip to content
Gospo FM Radio 99.1 FM, Ishara ya Upendo

Jinamizi la ajali watu watatu wafariki kwenye barabara kuu ya Nairobi-Mombasa.

27 Novemba 2026 · Kenya

Watu watatu wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa vibaya kufuatia ajali ya kugongana uso kwa uso kwenye barabara kuu ya Nairobi-Mombasa.

Watu watatu wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa vibaya kufuatia ajali ya kugongana uso kwa uso kati ya gari binafsi na lori la trela, karibu na ACK Salama kwenye barabara kuu ya Nairobi-Mombasa.

Kwa mujibu wa polisi wa trafiki, wahanga hao—wanaume wawili na mwanamke mmoja—walifariki papo hapo baada ya gari hilo binafsi, lililokuwa likielekea Mombasa, kugongana na lori la trela. Watu wawili waliojeruhiwa walikimbizwa katika Hospitali ya Sultan Hamud kwa ajili ya matibabu.

Dakitari mkuu kwenye kituo hicho cha kiafya Stephen Mwangangi maesema kuwa wawili hao walikuwa wakipata matibabu, ingawa mmoja wao, ambaye alipata majeraha mabaya kichwani, alihamishiwa Hospitali ya Makindu kwa ajili ya matibabu maalum.

Miili ya wahanga watatu waliofariki dunia imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Sultan Hamud.